CCMKK502_UTUNGAJI WA HATI ZA KIOFISI KATIKA KISWAHILI
Moduli hii inajumuisha notisi zote za daraja la tano na vitengo vitatu vinavyohusu utungaji wa hati za mawasiliano kwa namna mbalimbali. Moduli hii ina malengo yafuatayo : Kujadili mawasiliano mbalimbali ya kiofisi kupitia njia ya kuzungumza na kuandika katika shughuli za kazi, kutunga kimaandishi na kimazungumzo hati tofauti kwa kuzingatia kanuni na mitindo ya lugha ya Kiswahili ifaavyo, kuchambua kimazungumzo na kimaandishi hati za mawasiliano mbalimbali za kiofisi.kuwasilisha hati mbalimbali mahali zinapotakiwa.
Moduli hii itatoa mchango wa kujieleza kimawasiliano kwa kila mwanafunzi ambapo mwanafunzi atajieleza kupitia njia za mawasialano na kuandika hati mbalimabli kama vile barua ya kuomba kazi, barua ya kirafiki, ajenda , ripoti, wasifukazi wake na kadhalika.
Aidha, moduli itatoa mchango kwa mwanafunzi wa kutofautisha njia mbalimbali za mawasiliano na kuelewa umuhimu wake kwa jamii yoyote pia na kuelewa namna ya kuwasilisha hati mbalimbali kwa kutumia nyenzo mbalimbali tofauti.