Topic outline

 • CCMKK402 MATUMIZI YA KISWAHILI KATIKA MAWASILIANO YA KAWAIDA

  Utangulizi

  Moduli hii inalenga kumpa mwanafunzi ujuzi na uwezo vinavyostahiliwa ili mwanafunzi aweze kutumia Kiswahili kwa kuwasiliana kawaida kupitia matumizi ngeli za majina ya Kiswahili katika mawasiliano na kuwahudumia wateja na wageni wa kampuni, utungaji wa insha na matumizi ya istilahi/rejesta zitumikazo kimaandishi katika idara mbalimbali za kazi.

  Ili kuweza kutumia ngeli za majina ya Kiswahili katika mawasiliano na kuwahudumia wateja na wageni wa kampuni mwanafunzi ni lazima aweze kubainisha na kutumia vifaavyo ngeli za majina kulingana na aina za maneno ya Kiswahili. Kutumia vizuri vivumishi katika Ngeli za majina kulingana na mtindo wake katika Kiswahili na kutumia vyema viwakilishi katika Ngeli za Kiswahili kulingana na muundo wake kamili.

  Vile vile, mwanafunzi anahitaji kuwa mahiri wa kutunga sentensi bora za Kiswahili kulingana na muundo wake, kutunga aya na insha sahihi kwa kufuatilia muundo na aina yake katika Kiswahili na kutumia vizuri alama za Uakifishaji kulingana na matumizi yake kamili katika Kiswahili kwa kuhakikisha kuwa ana uwezo wa kutunga insha.

  Mwishowe, pamoja na ujuzi wa kupokea wageni/wateja vizuri kimazungumzo kwa kutumia rejesta mahususi, ujaza vizuri fomu za kikazi na kuandaa orodha kama inavyotakiwa katika idara fulani za kampuni na kueleza vizuri kazi na majina ya nafasi za kazi katika Kiswahili; mwanafunzi ataonyesha umahiri wa kutumia kimazungumzo na kimaandishi istilahi/rejesta zinazohusiana na kazi.